Duration 13:3

Jinsi ya kuanzisha biashara ya duka la vipodozi (How to start cosmetics shop business)

13 149 watched
0
113
Published 27 Sep 2021

Jinsi ya kuanzisha biashara ya duka la vipodozi ni muendelezo wa video zinazo tolewa na Tan Business Channel Je unafikiri uko tayari kuanzisha duka la vipodozi? Sasa hivi hapa Tanzania mahitaji ya vipodozi yameongezeka haraka sana. Kuna mahitaji ya aina nyingi za vipodozi kwa ajili ya wateja wa kipato cha kati na cha juu. Kabla hujaenda mbali na wazo la kuanzisha duka la vipodozi inabidi uwe na majibu ya maswali ya msingi kuhusu hiyo biashara. Biashara ya duka la vipodozi ina changamoto nyingi ukilinganisha na biashara nyingine. Kwa kuwa biashara ya duka la vipodozi ina changamoto nyingi, unashauriwa uanze polepole kulijaribu soko Usianze kwa nguvu bila ya kuwa na uhakika wa hali ya soko unalotaka kufanya biashara. Anza kuuza vipodozi kidogo kidogo kwa wateja ambao una walenga ili ufahamu muitikio wao kwa biashara yako. Hakikisha unatengeneza kundi maalum la wateja ambao watakuunga mkono wakati utakapoanza biashara kubwa ya duka la vipodozi.Ikiwezekana fanya haya majaribio kwa muda usio pungua miezi sita kusudi upate uhakika kuwa unaweza kufanya biashara ambayo itakuwa endelevu. Video inaeleza mambo 16 ambayo ni muhimu wakati wa kuanzisha biashara ya duka la vipodozi. Iwapo unataka ufafanuzi kuhusu mambo yaliyo elezwa kwenye video hii, basi wasiliana nami kupitia amwambola@gmail.com Sasa unaweza kununua vitabu vyetu vya ujasiriamali na bidhaa nyingine kupitia duka letu la online https://tanbusiness.myshopify.com

Category

Show more

Comments - 14