Duration 7:56

KARIBU NA WEWE ni wimbo uliokuwa kipenzi cha Watu wengi Duniani

2 004 watched
0
182
Published 16 Jul 2020

SOMA HAPA! Kurunzi letu leo hii linauangazia Wimbo uitwao Nearer, My God, to Thee au Karibu nawewe . Wimbo wa Tenzi No. 129. "Karibu na wewe" ni wimbo wa Tenzi ulioghaniwa na Sarah Flower Adams, ni Tenzi iliyojizolea umaarufu duniani kutokana na ukweli ambao bado baadhi ya watu wanavutana juu ya kuuamini kuwa ulikuwa ndiyo wimbo wa mwisho kabisa kutumbuizwa kwenye chombo cha muziki cha meli maarufu duniani Titanic kabla haijazama na kuua abiria wapatao 1,514 wakiwamo watoto 107 kufuatia kugonga jabali la barafu baharini usiku wa manane katika bahari ya Atlantic ya Kaskazini ya pata Aprili 15, 1912 hii ikiwa ni mwaka wa 71 tangu Tenzi Karibu na wewe kutungwa na Sarah Flower Adams aliyeishi kwa miaka 43 tu. Manusura katika ajali hiyo Violet Jessop alisema katika maelezo yake ya mwaka 1934 siku ya maafa hayo kuwa alisikia Karibu na wewe ikitumbuiza Sarah Flower Adams, alikuwa mpigania haki za wanawake [Namumini katika Mungu mmoja na siyo katika utatu mtakatifu] ambaye huyu alipatana na mchumba wake katika kipindi cha kuchumbiana kuwa hasingekuwa tayari kuwa Mama wa ndani tu, bali awe huru kujitokeza na kuhamasisha wanawake kutambua na kudai haki, uhuru na heshima yao toka kwa wanaume Dada huyu mshairi wa Ki-ingereza Sarah Flower Adams Tenzi hii aliighani mwaka wa 1841 huko nyumbani kwake Sunnybank, Loughton, Essex, England. Kwa kupendwa kwake huu wimbo waimbaji wengi walishiriki kuupa sauti tune tofauti tofauti ambapo awali kabisa ulipewa sauti na dada yake aliyeitwa Eliza. "Karibu na wewe pia uliimbwa na timu ya mabaharia na abiria waliokosa matumaini kwenye ajali ya meli ya SS Valencia ilipozama nje ya pwani ya kisiwa cha Vancouver Canada mnamo mwaka ule wa 1906, na pia Meli Ya Titanic mwaka 1912 na mabaharia wakapabatiza jina kama kaburi la baharini la Pacific. Kuna ushuhuda mwingine wa tenzi hii kuwa Rais wa 25 wa Marekani William McKinley yapata Septemba ya mwaka 1901, maneno yake ya mwisho wa uhai wake yalitokana na mistari michache ya kwanza ya Karibu na wewe. Majira ya saa 9:30 alasiri ya Septemba 14, 1901, baada ya kimya cha dakika tano kilichotanda taifa zima, bendi kadhaa za Marekani zilitumbuiza Karibu na wewe ambao ulikuwa kipenzi cha Rais McKinley katika kumbukumbu zake. uliimbwa na bendi kwenye mtaa maarufu wa Pennsylvania Avenue unaounganisha White House na mji mkuu wa Marekani Washington D.C. wakati wa shughuli za mazishi na hitimisho la ibada ya msiba na katika ibada kama hiyo kwa heshima yake huko Westminster Abbey, London. Pia ulitumbuizwa wakati mwili wa Rais wa 20 wa Marekani aliyeuawa James Abram Garfield ukishushwa kaburini huko Lakeview Cleveland, Ohio, huyu Kiongozi aliwahi kuwa Mhubiri, Mwanasheria kitaaluma, Mwalimu, Mzee wa Kanisa na alikuwa askari mwenye cheo cha Meja Jenerali aliyepigana vita mbalimbali. Pia Karibu na wewe uliimbwa wakati wa msiba wa Rais wa 38 wa Marekani Gerald R. Ford na kwenye msiba wa Prince Bernhard mwana wa Malkia wa The Netherlands. Ndugu Ted Turner, akiongea muda mfupi kabla ya uzinduzi wa televisioni yake maarufu duniani ya CNN mwaka 1980 jijini Atlanta Marekani, aliahidi kuwa: “Kama siyo matatizo ya kiufundi, hatutaacha kwenda hewani mpaka dunia itakavyoisha.” Tutakuwa hewani, na tutarusha hewani tukio la jinsi dunia itakavyokuwa inatoweka laivu, na hilo litakuwa tukio letu la mwisho.... na mwisho huo wa dunia utakavyokuja, tutarusha hewani wimbo “Nearer My God to Thee/Karibu na wewe” kabla mitambo yetu ya kurusha matangazo haijazimika na kutoweka." Ndugu mfuatiliaji wa kipindi hiki cha kurunzi la tenzi unaweza kutoa maoni na ushauri kwa ku comment na pia usisahau ku like na ku Subscribe channel hii ili tuweze kukuhabrisha kwa vipindi vinavyoendelea Mtayarishi ni Douglas Orical Majwala na Msimulizi wako ni Emmanuel Shedo

Category

Show more

Comments - 39